Hali ya Duke Abuya yadaiwa kuwa mbaya
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa taarifa ya awali kutoka kwa daktari wa timu hiyo, Moses Etutu, inaeleza kuwa kiungo Duke Abuya ameumia sehemu ya nyama za paja.
Abuya alipata jeraha hilo baada ya kuchezewa rafu ambayo Yanga imeielezea kuwa mbaya sana na Libasse Gueye, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga na Simba uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Uhuru majira ya saa 1 usiku.
