Haji Manara afurushwa rasmi Yanga

Aliyekuwa Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara, ameonyesha kuchukizwa na kauli za baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo wanaodai kuwa wachezaji wa Simba walichoma sindano za kusisimua misuli, kitu ambacho wanaamini kiliidhoofisha timu yao na kuwafanya wapoteze mchezo wa juzi Jumamosi, Oktoba 10, 2026.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kukwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa kufikisha pointi 21, huku Yanga ikishushwa hadi nafasi ya pili ikibaki na pointi 18.

Manara ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika baadhi ya mambo ambayo anaamini hayana mashiko kufuatia madai hayo ya mashabiki, na amewataka kukubali kuwa timu yao ilizidiwa kimchezo.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons