Gamondi kubwaga manyanga Stars kisa Yanga
Kocha wa Taifa Stars, Miguel Gamondi, ameripotiwa kususia mazoezi na kutishia kuacha kuifundisha timu hiyo baada ya TFF kukubali ombi la Yanga la kuwarejesha kambini wachezaji wake wanne muhimu baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya FAR Rabat.
Gamondi analalamika kutoshirikishwa katika maamuzi hayo na kuhoji kwa nini wachezaji wa Simba, Azam na Singida wamebaki kambini huku wa Yanga wakiondoka.
Taarifa hizi zimetolewa na Jemedar Said
