Gamondi ahusishwa kurejea Yanga


Dalili zinaashiria kuwa safari ya Manqoba Mngqithi ndani ya Yanga SC huenda isiendelee hadi mwisho wa msimu, huku uongozi wa klabu hiyo ukiendelea kumuweka chini ya uangalizi mkubwa kufuatia vikao vilivyofanyika kuhusu mwenendo wa timu.

Taarifa zinaeleza kuwa Manqoba amepewa muda zaidi wa kujirekebisha, jambo linaloongeza presha ya kuhakikisha matokeo yanaridhisha uongozi na mashabiki wa Wananchi.

Wakati hali hiyo ikiendelea, jina la Miguel Gamondi, kocha wa zamani wa Yanga na kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, linatajwa kuwa miongoni mwa chaguo la kwanza iwapo klabu itaamua kuachana na Manqoba.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons