Daudi Kanuti afariki dunia

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Lameck Nyambaya ametangaza kwa masikitiko kifo cha kiongozi mwenzao Mzee Daudi Kanuti, kilichotokea usiku wa Oktoba 17, 2026.

Marehemu Mzee Daudi Kanuti alikuwa mtumishi wa DRFA kutoka Ofisi ya Sekretarieti, na pia alikuwa akihudumu kama Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ilala (IDFA).

Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 17, 2026 na Ofisi ya Mwenyekiti ya DRFA imeeleza kuwa, enzi za uhai wake, marehemu alikuwa kiongozi, baba, na mlezi wa karibu na kueleza kuwa “Mchango wake mkubwa katika utumishi wa DRFA na maendeleo ya soka kwa ujumla utabaki kuwa kumbukumbu ya kudumu ya daima.”

Taarifa zaidi kuhusu ratiba ya mazishi na taratibu nyingine za msiba huu zitatolewa rasmi kadri zitakavyopatikana kutoka kwa familia na uongozi wa DRFA.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons