Cedric Kaze yuko mzigoni
Kocha mkuu wa Kagera Sugar, Cedrick Kaze, anaendelea na kazi ya kukiandaa kikosi chake kuelekea mechi za Ligi Kuu ya NBC zitakazorejea baada ya michezo ya kimataifa ya kalenda ya FIFA.
Kaze alikabidhiwa jukumu la kuliongoza benchi la ufundi la Kagera Sugar baada ya kuondoka kwa Juma Kaseja wiki iliyopita.
Kocha huyo raia wa Burundi anakiandaa kikosi chake katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera kwa ajili ya mechi ijayo ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City FC itakayopigwa Oktoba 9, 2026 kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.



