Yanga bado hawatufikii- Katwila

Kocha mkuu wa klabu ya Geita FC, Zuberi Katwila, baada ya mchezo kumalizika kwa bao 1-0 dhidi ya yanga SC.amekiri kuwa klabu ya Yanga SC bado ina safari ndefu kwenye mpira. Amesema hayo baada ya mchezo alioutumia mbinu kubwa ili kupata matokeo,

“Klabu ya Yanga bado hawana uwezo wa kutufikia sisi, yani hata kidogo. Hata wakipata bao, basi ni kwa bahati sana. Nimependa tulivyolinda nafasi pamoja na uwezo wa wachezaji wangu. Mfumo wao niliweza kuudhibiti. Hata kupata kadi ni sehemu ya mchezo, sio kwamba wamefanya vibaya, hapana, hii ni moja ya changamoto.”

“Kwa upande wangu, niwapongeze wapinzani wangu. Safu yao ya ulinzi ilikuwa imara zaidi kuliko sisi, ila kwa uwezo wetu tumefanya makubwa. Walijua wakija watafanya makubwa au kupata mabao zaidi, lakini wamekuta matokeo yamekuwa kama haya.”.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI