Viongozi Yanga waenda kumfariji Pacome
Sehemu ya Idara ya Habari ya Yanga SC ikiongozwa na Meneja Habari na Mawasiliano wake Ally Kamwe, imemtembelea nyota wao Pacome Zouzoua nyumbani kwake na kumkabidhi mahitaji mbali mbali.
Kwa mujibu wa Kamwe, nyota huyo huenda akawepo katika dimba la Azam Complex, Chamazi kuushuhudia mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Gaborone United.
Mechi itapigwa Jumamosi ya Septemba 12, 2026 saa 1:00 usiku.






