Tutabeba ubingwa wa bara- Barker
Kocha Barker akielezea umuhimu wa kambi ambayo tumeiweka Afrika Kusini na ushirikiano mkubwa ambao anatoa Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji, kwa kikosi chake, ikiwepo kulipa gharama zote za kambi hii.
“Nahitaji kuondoka Simba SC nikiwa nimeipa ushindi ambao haujawahi kupatikana kwa takribani misimu 5.
Nahitaji kuifanya iwe ya mfano ndani ya ligi ya Tanzania. Msimu uliopita nilipata nafasi ya kufanya vizuri, licha ya timu nilikuta ikiwa katika nyakati mbovu.
Ila kwa msimu huu, Mungu asaidie tu, maana nilichopanga ni kuwafanya mashabiki wa Simba SC waongezeke, hata wale waliokata tamaa wanaweza kurudi.
Uwezo wangu mimi naujua, si kama wao, kila mtu ana uwezo wake. Ndiyo maana kila timu ina shida zake. Nahitaji kufanya jaribio la mechi za kirafiki hapa nchini Afrika Kusini kwa kipindi tulichoweka kambi huku.
Mimi niseme Rais wetu amejua nini tunahitaji, ndiyo maana tumepewa heshima ya kupewa kambi mbali na Tanzania. Huu ni mwanzo mzuri kabisa.
Lile kombe moja tulilobeba sio kwamba ndiyo tumemaliza, hapana, ila tunahitaji kufanya makubwa kwenye Ligi Kuu NBC. Wengi wanasema kuwa tunaweza kuwa na presha juu ya mchezo wetu dhidi ya Yanga SC, ambao ni wapinzani wetu wakubwa, ila niwaambie hakuna presha yoyote. Mpira utachezwa na ubingwa juu.”
