TRA United na Mexime kimeeleweka
TRA United imefanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi baada ya kuachana na Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije, huku Mecky Maxime akitarajiwa kuchukua nafasi hiyo.
Ndayiragije ameondoka katika klabu hiyo baada ya uongozi wa TRA United kutangaza kusitisha ushirikiano wake na kocha huyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Maxime tayari yupo njiani kujiunga na kikosi cha TRA United, ambako anatarajiwa kuanza majukumu yake mapya baada ya kukamilika kwa taratibu za mwisho.
Maxime anarejea kwenye benchi la ufundi baada ya kuwa nje ya kazi ya ukocha kwa kipindi fulani, huku akitarajiwa kuiongoza TRA United katika hatua inayofuata ya msimu.
Mabadiliko hayo yanakuja wakati TRA United ikihitaji kurekebisha mwenendo wake na kuongeza ushindani katika mashindano ya msimu huu.
