Tanzania, Kenya na Uganda kupokwa uenyeji AFCON
Hivyo Awali ilipangwa kufanyika nchini Kenya, Tanzania na Uganda, lakini mashindano hayo yanaweza kurudishwa au kuhamishiwa kwingine kutokana na kuchelewa kwa miundombinu na maandalizi.
Inadaiwa CAF tayari imewasiliana na baadhi ya nchi zenye uwezo wa kuandaa mashindano hayo kwa muda mfupi: Morocco Algeria na Afrika Kusini .
Ndani ya CAF, baadhi ya wajumbe wanadaiwa kuwa na matumaini madogo kuhusu nchi hizo tatu kuwa tayari kwa wakati.
Hali hii inatofautiana na msimamo rasmi wa Rais wa CAF, Patrice Motsepe, ambaye amesema hakuna “Plan B wala Plan C” kwa AFCON 2027
