Seif Karihe atambulishwa Mtibwa Sugar
Klabu yenye historia kubwa kwenye soka la Tanzania, Mtibwa Sugar, imetangaza rasmi usajili wa mshambuliaji hatari Seif Karihe, ambaye ametua klabuni hapo akitokea Mashujaa FC ili kuongeza makali kwenye safu yao ya ushambuliaji.
Uongozi wa Mtibwa Sugar umeridhishwa na uwezo wa mshambuliaji huyo, wakiamini uzoefu wake utasaidia kwa kiasi kikubwa kwenye mashindano ya ligi.
Kupitia kauli mbiu yao ya “United WeStand”, wakazi wa Turiani na familia nzima ya Wana-Manungu wamemkaribisha mchezaji huyo kwenye "nyumba ya vipaji."
