Sakata la Makonda na Sandaland lafikia hivi
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema kuna nafasi ya kuboresha jezi za timu ya Taifa kupitia kipengele kilichopo kwenye mkataba wa mzabuni wa jezi.
Makonda amesema mkataba huo una kipengele kinachotaka kila mwaka kukaa na kupitia performance ya mzabuni, akieleza kuwa hilo linaweza kuwa fursa ya kuboresha muonekano wa jezi za timu ya Taifa.
“Ukisoma mkataba wa mzabuni wa jezi za timu ya Taifa kuna kipengele kinataka kila mwaka kukaa na kupitia performance yake. Nikaona hapo ndio kuna nafasi ya sisi kuboresha jezi zetu.” Makonda amesema jezi ya timu ya Taifa haipaswi kuonekana kama vazi pekee, bali pia ni sehemu ya kuitangaza na kuitambulisha Tanzania.
“Jezi ya timu ya Taifa sio tu vazi, ni kitu kinachoitangaza na kuitambulisha nchi! Kupitia jezi tunapaswa kuiuza nchi kupitia jezi yetu.” Akizungumzia jezi zilizotambulishwa, Makonda amesema:
“Jezi za timu zilizotambulishwa ni mbaya! Huo ndio ukweli, hata wakizipiga dodoki vipi jezi ni mbaya.” Paul Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
