Pacome awatakia kila kheri Yanga
Kiungo mshambuliaji aliyekwenye maumivu Pacome Zouzoua amewatumia salamu Watanzanis hasa klabu yake ya Yanga.
"Kila la kheri familia nzima ya Yanga kwenye safari ya Ligi ya Mabingwa. Isivyo bahati kutokuwepo kwangu kunanizuia mimi kuwa nanyi dimbani, lakini moyo wangu na fikra zipo pamoja nanyi”
Ni sehemu ya andiko la nyota wa Yanga SC, Pacome Zouzoua akiitakia heri timu yake ambayo leo itaanza mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United ya nchini Botswana.
Pacome amewataka wachezaji wenzake kujitoa kwa kila hali ili kuipambania jezi yao na kuongeza kuwa atakuwa pamoja nao hata kama yeye yupo mbali.
