Niffer atangaza kudata kwa Libasse Gueye
Mfanyabiashara na mrembo maarufu nchini, Niffer, ameshangaza watu kwa maranyingine baada ya kuanza kuonyesha hadharani mahaba na ukaribu wake kwa winga hatari wa Simba SC raia wa Senegal , Libasse Gueye.
Licha ya Niffer kufahamika kama shabiki lialia wa Yanga SC, mrembo huyo amezua mshtuko kwa mashabiki baada ya ku-repost post mbili za Gueye siku ya leo pekee.
Huku akiweka comments zilizozua maswali mengi ikiwemo kumwita "Top Simba SC treasure" akimaanisha "Hazina kuu ya Simba SC" na kuandika kuwa anamkubali popote alipo huku akimuombea afike mbali zaidi.
Gueye anaendelea kuthibitisha kuwa yeye ni X-Factor wa Simba SC msimu huu, baada ya kutangazwa Mchezaji Bora wa Agosti kwa kuhusika kwenye mabao 6 ya Ligi Kuu, leo amefunga mabao mawili dhidi ya Mighty Wanderers kwenye ushindi wa 6-1.
