Ndayiragije atupiwa virago TRA

Klabu ya TRA United SC imethibitisha kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha mkuu Etienne Ndayiragije kwa makubaliano ya pande zote mbili kuanzia Septemba 7, 2026.

Taarifa hiyo iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo huku ukimshukuru kwa dhati Kocha Ndayiragije kwa mchango wake mkubwa, weledi, na huduma ya kipekee aliyoitoa kwa timu katika kipindi chote alichokuwa sehemu ya klabu hiyo na kumtakia kila la kheri na mafanikio mema katika hatua inayofuata ya maisha na taaluma yake ya ukocha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo TRA United itaendelea kuwasiliana na wanachama, mashabiki, na wadau wake kuhusu hatua zaidi zinazohusiana na uongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo.

Kocha huyo ameondolewa kwenye nafasi hiyo kufuatia mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo ambayo imekusanya alama tatu kwenye michezo mitano huku ikishindwa kupata ushindi, vipigo viwili na sare tatu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI