Mzize, Job safi Yanga

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe, amesema nyota wa timu hiyo Clement Francis Mzize na Dickson Job wako katika hali nzuri na hivi karibuni wataanza tena mazoezi na timu. Wachezaji hao walifanyiwa check-up nchini Afrika Kusini na baada ya kuruhusiwa, sasa wanatarajiwa kurejea kwenye mazoezi rasmi.

Kurejea kwa Mzize na Job ni nyongeza kubwa kwa Yanga, kwani timu hiyo inapata nguvu mpya kwenye safu ya ushambuliaji kupitia Mzize na kwenye ulinzi kupitia Job. Kwa mashabiki wa Yanga, kurejea kwa nyota hao wawili ni kama usajili mpya katikati ya msimu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI