Mwanasheria wa Sandaland aingilia kati suala la jezi za Stars
Mwanasheria wa kampuni ya Sandaland, Advocate Nziku, amesema TFF ilikuwa na nafasi ya kukataa sampuli za jezi endapo hazikukidhi viwango, kwa mujibu wa Ibara ya 5(6) ya mkataba kati ya pande hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Nziku amesema ibara hiyo inampa nafasi ya kutoa mapendekezo kuhusu uzi na muundo wa jezi, huku uamuzi wa mwisho ukiwa mikononi mwa TFF.
Amesisitiza kuwa changamoto zozote za kimkataba zinapaswa kushughulikiwa kwa kuzingatia masharti yaliyomo katika mkataba huo.
