Mwanariadha wa Tanzania apongezwa na Ubalozi Ujerumani


Mwanariadha wa Tanzania, Gabriel Geay amepokelewa na kupongezwa katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani baada ya kutwaa medali ya shaba katika mbio za BMW Berlin Marathon 2026.

Geay amefikisha heshima hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio hizo zilizofanyika Berlin Septemba 27, 2026, akiiwakilisha Tanzania katika moja ya mashindano makubwa ya marathon duniani.

Akizungumza wakati wa kumpokea Geay, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Hassani Mwamweta amempongeza kwa matokeo hayo na kumtia moyo kuendelea na maandalizi ili kupambania nafasi ya kwanza katika mashindano yajayo.

Mwamweta pia amesema amefanya mazungumzo na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu kuongeza idadi ya wanariadha kutoka Tanzania watakaoshiriki mashindano ya kimataifa, ikiwemo BMW Berlin Marathon, hatua inayolenga kutoa nafasi zaidi kwa vipaji vya Tanzania kushindana kwenye majukwaa makubwa ya riadha.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI