Mimi ni Simba lialia- Manara

Mimi kama mwanahabari na msemaji wa timu ya taifa pamoja na vilabu vyote Tanzania, nitajiunga na Simba SC kwenda kupambana ili tupate ubingwa na turejee nao tukiwa kidedea. Nasema hivyo sio kwa ubaya, hapana, nasema hivyo kulingana na kazi yangu ninayoifanya.

Siwezi kwenda Yanga nimevaa uzi wa Yanga endapo mimi ni mwana Yanga SC, ila nitazuru mechi zote za timu zote nikiwa na jezi ya timu ya taifa. Basi, furaha sitokosa. Nafanya hivyo kwa sababu nyie waandishi wa habari mna tabia moja. Unaweza kukuta nashangilia Simba SC kupata ubingwa, mnakamua kukata kipande kimoja cha video kikinionyesha nimeshangilia Simba na mkasema nimehama timu yangu, nimerudi Simba SC.

Mechi zote nitashiriki, mpaka ya Singida BS nitakuwa pamoja na nyie. Siwezi kuwaangusha mashabiki wote wa Tanzania. Nataka niweke hii kwa maana kuna kitu wengi wana-noti kuwa nitavaa jezi ya Singida. Hapana, yaani jezi ni ile ile ya Tanzania, timu ya taifa.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI