Mchezaji wa zamani Simba afariki dunia
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba SC Bakari Iddi amefariki dunia arasiri mitaa ya nyumbani kwake Kigogo jijini Dar es Salaam.
Ndugu wa marehemu Andi Iddi Bakari na Gharib Bashiru wameujuza mtandao wa Mambo Uwanjani Blog kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Simba miaka ya 1990 hatunaye.
Ikumbukwe Iddi alikuwemo katika kikosi cha Simba kilichotwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika mashariki na kati, maarufu kombe la Kagame Cup mwaka 1991 kilichoifunga SC Villa ya Uganda mabao 3-0.
Mwili wa marehemu umepelekwa hospitali na taratibu za mazishi zitafanyika mara baada ya kupangwa na familia.
Innalillah wainnailayh raajiun
