Mbunifu wa jezi za Yanga, aibukia Chelsea
Aliyekuwa mbunifu rasmi wa jezi za Yanga SC na Zanzibar Heroes, Sheria Ngowi, amezua gumzo mtandaoni baada ya kuonyesha jinsi jezi alizobuni nyuma zilivyotangulia mitindo kabla ya makampuni makubwa duniani kama Nike, Adidas, na Macron kuitumia hivi karibuni.
Chelsea FC vs Yanga SC: Mtindo wa mawingu/madoa ya bluu aliotengeneza kwenye jezi ya Yanga SC (2023/24) unafanana na ule uliotumiwa na Nike kwa Chelsea FC (2026/27).
PSG vs Yanga SC: Muundo wa mistari inayopishana aliozindua Yanga SC (Julai 2022) uliitangulia jezi ya PSG x Jordan (Januari 2023).
Crystal Palace vs Yanga SC: Jezi ya dhahabu yenye ukola aliyoibuni kwa Yanga SC (Novemba 2024) ilitoka kabla ya Macron kuitumia kwa Crystal Palace (Agosti 2025).
Argentina vs Zanzibar Heroes: Nakshi za urembo kwenye jezi ya Zanzibar Heroes (2024) zinafanana na muundo mpya wa Adidas kwa Argentina 🇦🇷 (2026).
NOTE: Ngowi anadhihirisha kuwa kazi za wabunifu wa nyumbani zina kiwango cha kimataifa na zimekuwa zikiongoza mitindo duniani (setting global trends).




