Mayele azikwepa timu za Tanzania bara

Nyota wa Al Ahly Tripoli na mshambuliaji wa zamani wa mabingwa wa Tanzania, Young Africans (Yanga SC), Fiston Mayele, amesema hatamani kukutana na timu kutoka Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika hatua zinazofuata za mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mayele amesema sababu ni kwamba timu za Tanzania zina kelele nyingi tofauti na timu kutoka Zanzibar. Pia ameeleza kuwa kipindi alipokuwa akiichezea Pyramids, hakuwahi kukutana na timu za Tanzania na alifurahia hali hiyo.

“Sitaki kukutana na timu za Tanzania kwa sababu timu za Tanzania zinakelele sana tofauti na Zanzibar. Kipindi nilipokuwa Pyramids, sikuwahi kukutana na timu za Tanzania na nilifurahi sana.

Pia kuna watu nilikuwa na mawasiliano nao pale Yanga, marafiki zangu, nilikuwa nawaambia sitaki kukutana na timu za Tanzania.”


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI