Maulid Kitenge atua redio Uhuru
Mkongwe wa habari nchini, Maulid Kitenge, amejiunga na kituo cha redio cha Uhuru FM, baada ya hapo awali kufanya kazi kama mtangazaji wa Wasafi FM.
Kitenge, ambaye ni miongoni mwa watu wenye uzoefu mkubwa katika tasnia ya habari na utangazaji nchini, alikuwa kimya kwa muda na kutokuwepo kwenye kituo cha Wasafi FM hali iliyozua maswali miongoni mwa wasikilizaji na wafuasi wake.
Hatua yake ya kujiunga na Uhuru FM inatajwa kuwa ni mwanzo wa sura mpya katika safari yake ya utangazaji, huku mashabiki na wasikilizaji wakisubiri kujua nafasi atakayopewa pamoja na vipindi atakavyokuwa akivisimamia katika kituo hicho.
