Makonda azigomea jezi mpya Taifa Stars
Makonda akataa jezi alizozivaa Naibu Waziri wake FA asema “ofisi yangu haina taarifa,tuheshimiane”
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amezikataa jezi mpya za Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, zilizozinduliwa rasmi leo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram,
Makonda ameposti picha za jezi hizo na kueleza kuwa hazikidhi kiwango anachokitarajia kwa timu ya taifa, huku akisema ofisi yake haikuwa na taarifa kuhusu matumizi ya picha za Naibu Waziri katika suala hilo.
"Hii sio jezi ya Taifa Stars. Taifa Stars kwa ubora wake hatuwezi kuwa na jezi za kiwango cha chini hivi. Acheni kutumia picha za Naibu wangu huku ofisi yangu haina taarifa. Tuheshimiane," ameandika Makonda.
