Makonda awakutanisha vigogo Simba
Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, pamoja na Wajumbe wa Bodi wanaotokea upande wa Mo Dewji, wote wapo Arusha muda huu baada ya kupokea wito kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda.
Leo Septemba 29, 2026, Waziri Makonda amewaita viongozi hao wa Simba SC kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea ndani ya klabu hiyo.
Inaelezwa kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili namna ya kupanga maendeleo ya soka nchini Tanzania, pamoja na kuhakikisha heshima na nidhamu ya mchezo wa soka vinaendelea kulindwa.
