Madee kuanzisha redio ya kupiga nyimbo za zamani
Msafara wa Wakongwe wa Muziki wa Bongo Fleva upo njiani kuelekea Arusha kwa ajili ya Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva linalotarajiwa kufanyika Septemba 19, 2026 katika Viwanja vya General Tyre.
Akizungumza akiwa njiani kuelekea Arusha, Mratibu wa Tamasha hilo, Madee Ali amesema baada ya tamasha kumalizika, mpango unaofuata ni kufungua redio maalumu itakayokuwa ikipiga nyimbo za zamani (Old School).
Aidha, Madee amewataka Wakazi wa Arusha kujiandaa kwa tamasha hilo, akisema wamewaletea burudani yenye kila kitu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea safari ya miaka 30 ya Bongo Fleva.
