King Kinya afariki dunia

Tasnia ya uchoraji katuni nchini imepata pigo baada ya kifo cha Kinyagulo Tuzo, maarufu King Kinya, aliyefariki dunia Septemba 17, 2026 baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.

Kifo cha King Kinya kimethibitishwa na Ofisi ya Rasilimali Watu ya Kampuni ya MCL, aliyokuwa akiifanyia kazi kama mchora katuni wa magazeti.

Kaka wa marehemu, Kiondo Mjema, amesema King Kinya alianza kuugua akiwa nyumbani Tabata mwanzoni mwa Julai mwaka huu, kabla ya kupelekwa Morogoro baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya.

Amesema akiwa Morogoro, marehemu alipelekwa hospitalini na kulazwa kwa takriban wiki moja, kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbani huku akielekezwa kurejea hospitalini kwa ajili ya ufuatiliaji.

Kwa mujibu wa Kiondo, King Kinya alirejea hospitalini juzi baada ya kusumbuliwa na tumbo, kuharisha na kutapika, lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya usiku wa kuamkia jana, Septemba 15, akilalamikia maumivu makali ya tumbo na kichwa. Amesema msiba upo Kimara Kona.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI