Kante apata timu Algeria
Aliyekuwa kiungo wa Simba SC, Alassane Kanté ametangazwa rasmi kama mchezaji mpya wa klabu ya JS EI Biar inayoshiriki Ligi Kuu ya Algeria (Ligue 1) kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na Simba SC kwa maslahi ya pande zote mbili.
Kante (25) raia wa Senegal amesaini mkataba wa miaka miwili utakaombakisha kwenye klabu hiyo iliyopanda daraja msimu huu kwenda Ligue 1 ikitokea Ligue 2 mpaka Juni 2028.
