Kangwanda aitwa timu ya taifa
Kocha wa Zambia, George Lwandamina, ameitangaza orodha ya wachezaji kwa ajili ya michezo ya kufuzu AFCON.
Albert Kangwanda wa Yanga SC ameitwa kwenye kikosi cha Chipolopolo, huku Clatous Chama wa Simba SC akikosa nafasi.
Hii ni habari kubwa kwa Kangwanda ambaye anaendelea kujenga nafasi yake kwenye timu ya taifa.
Kwa upande wa Chama, kuachwa nje ni pigo jingine na sasa itakuwa juu yake kuendelea kufanya kazi ili kurejea kwenye mipango ya kocha.
