Kaka yake Kibabage apandishwa cheo Marekani

Mogaj Kibabage, kaka wa mchezaji wa Simba SC, Nickson Kibabage, amepandishwa cheo kutoka Koplo (Corporal) hadi Sargent (Sergeant) katika Jeshi la Marekani (US Army).

Mogaj amefanikiwa kupata cheo hicho baada ya kufaulu kozi maalumu ya kijeshi iliyomuwezesha kustahili kupandishwa cheo.

Kupitia ukurasa wake wa Threads, Mogaj ametuma salamu kwa familia yake huku akiwashukuru kwa kumuombea na kumpa nguvu wakati wote alipokuwa akipitia mafunzo ya kozi hiyo.

Hongera sana Mogaj Kibabage kwa hatua hii kubwa


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI