Kagera Sugar yatambulisha benchi lake la ufundi
Klabu ya Kagera Sugar FC imemtangaza Amri Kiemba kuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo.
Kiemba ambaye amewahi kuitumikia Kagera Sugar kama mchezaji ataenda kuungana na Kocha Mkuu Cedric Kaze, pamoja na Frank Domayo ambaye ametangazwa kuwa Kocha Msaidizi Namba Mbili.
Katika hatua nyingine ya kuboresha benchi lake la ufundi, Kagera Sugar imemtangaza Kefa Mabadil kuwa Mchambuzi wa Video (Video Analyst) wa klabu hiyo.
Benchi la Ufundi:
▪️ Cedric Kaze — Kocha Mkuu
▪️ Amri Kiemba — Kocha Msaidizi
▪️ Frank Domayo — Kocha Msaidizi Namba Mbili
▪️ Kefa Mabadala — Mchambuzi wa Video
