Kadi nyekundu ya Sillah yafutwa

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefuta adhabu ya kadi nyekundu aliyooneshwa mchezaji wa Azam FC, Gibril Sillah, katika mechi dhidi ya Kagera Sugar, baada ya kujiridhisha kupitia picha jongeo na taarifa ya wataalamu kuwa mchezaji huyo hakustahili adhabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TPLB, uamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia Kanuni ya 12:8 ya Ligi Kuu kuhusu usimamizi wa ligi.

Aidha, mwamuzi wa akiba wa mchezo huo, Greyson Buchard kutoka Kagera, amepewa onyo kali kwa kosa la kuonyesha mapungufu ya kiuchezaji yaliyotokana na kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars, Hussein Massanza, ametozwa faini ya shilingi milioni 10 kwa kosa la kumshutumu na kumtolea lugha ya matusi mwamuzi wa kati wa mchezo kati ya Singida BS na Simba SC kupitia chapisho moja la mtandaoni, kinyume na kanuni za Ligi Kuu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI