Idara ya masoko Yanga yabisha hodi Vodacom
Idara ya Wanachama na Masoko leo imetembelea Ofisi za Vodacom Tanzania kwa ajili ya zoezi la usajili wa wanachama sambamba na kuimarisha Tawi la Yanga Vodacom.
Zoezi hili ni sehemu ya mkakati wa Klabu wa kuwafikia Wananchi katika taasisi, makampuni na maeneo mbalimbali ya kazi ili kuwawezesha kujiunga na familia ya Yanga na kuendelea kuwa sehemu ya safari ya Klabu popote walipo.
Tunawashukuru uongozi pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwa mapokezi mazuri na ushirikiano wao katika kufanikisha zoezi hili.


