Hii ndio Simba
Bao pekee lililofungwa na Anicet Oura limeiwezesha Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Might Wonderers katika uwanja wa Bingu, Lilongwe nchini Malawi jioni ya leo.
Mchezo huo wa Ligi ya mabingwa Afrika mkondo wa kwanza, unaifanya Simba kusubiri mchezo wa marudiano utakaofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kutoka sare yoyote Ili isonge mbele raundi ya kwanza.
Shukrani wachezaji wa Simba Kwa kujituma ugenini na kuweza kupata ushindi.
