Gor Mahia yasimamisha wachezaji kisa kipigo cha Pyramids
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia, wamewasimamisha baadhi ya wachezaji kufuatia kipigo cha mabao 5-1 dhidi ya Pyramids katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Gor Mahia walitolewa kwenye mashindano hayo kwa jumla ya mabao 7-1 baada ya michezo miwili dhidi ya Pyramids.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani, uamuzi huo umefikiwa na uongozi wa klabu hiyo kutokana na wasiwasi kuhusu kiwango na mwenendo wa baadhi ya wachezaji kufuatia kipigo hicho.
