Gamondi atangaza kikosi, Mwalimu wa Yanga ndani
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Miguel Ángel Gamondi, ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji watakaoingia kambini kujiandaa na michezo ya kufuzu Ligi ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 dhidi ya Guinea Bissau na Madagascar, pamoja na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Ghana.
Makipa: Zuberi Foba (Azam FC), Aishi Manula (Azam FC), Yona Amos (Singida BS), Metacha Mnata (Singida BS), Hussein Masalanga (Young Africans).
Mabeki: Ibrahim Bacca (Young Africans), Bakari Mwamnyeto (Young Africans), Lameck Lawi (Azam FC), Twalib Nuru (Azam FC), Vedastus Masinde (Simba SC), Mohammed Mussa (Young Africans), Danillo Maino (FK Panevezys, Lithuania), Haji Mnoga (Patro Eisden, Ubelgiji), Bakari Msimu (Simba SC), Nickson Kibabage (Simba SC), Mohammed Hussein (Young Africans), Anthony Mligo (Simba SC), Pascal Msindo (Azam FC), Nathaniel Chilambo (Simba SC).
Viungo: Novatus Miroshi (Göztepe, Uturuki), Himid Mao (Azam FC), Adolph Mtasingwa (Kaizer Chiefs, Afrika Kusini), Yusuf Kagoma (Simba SC), Mohamed Sagaf (Eastbourne Borough, Uingereza), Alphonce Mabula (JS Kabylie, Algeria), Charles Mmombwa (Zabbar, Malta), Mudathir Yahya (Young Africans), Feisal Salum (Azam FC), Sheikhan Khamis (Singida BS), Morice Abraham (Simba SC), Abdulkarim Kiswanya (Azam FC).
Washambuliaji: Tarryn Allarakhia (Boreham Wood, Uingereza), Simon Msuva (Newroz, Iraq), Bernard Kamungo (FC Dallas, Marekani), Kelvin John (Aalborg, Denmark), Kibu Dennis (Al Nasr, Libya), Abdul Suleiman (Azam FC), Sabri Kondo (Hacken, Sweden), Cyprian Kachwele (HFX Wanderers, Canada), Said Khamis (Unattached), Selemani Mwalimu (Young Africans), Paul Peter (JKT Tanzania).
Uteuzi huu unalenga kutengeneza kikosi shindani kitakachohakikisha Tanzania inaanza vyema kampeni yake ya kusaka nafasi ya kushiriki AFCON 2027, huku mchezo wa kirafiki dhidi ya Ghana ukitumika kama kipimo sahihi cha kuimarisha ushirikiano na mbinu za timu kabla ya michezo hiyo ya ushindani.
