Gamondi amtaja Manula
Kocha Mkuu wa Taifa Stars amesema Aishi Manula ana majeraha, hivyo hawezi kuitwa kwa sasa, huku akisisitiza kuwa anaendelea kuwa na imani na makipa waliopo.
Gamondi pia amesema mashabiki wanaweza kulalamika kwa kuwa wana hisia zao, lakini yeye hawezi kufuata kila kinachosemwa na mashabiki.
"Manula alikuwa kwenye orodha, lakini aliumia. Ninaendelea kuwa na imani na mlinda mlango aliyepo,” alisema Gamondi.
