Ferooz atingisha na Starehe
MSANII wa Bongo Fleva, Feruzi Mrisho Rehani 'Ferooz' amesema kila anapopanda jukwaani na kuimba wimbo wa Starehe unakuwa na mapokeo makubwa kama ameuandika hivi karibuni, wakati una miaka zaidi ya 21.
Ferooz aliliambia Mwanaspoti namna miaka 30 ya Bongo Fleva inavyowakutanisha na jamii pamoja na mashabiki wao, jinsi inavyowapa picha ya jamii bado inahitaji kusikia ujumbe unaowagusa moja kwa moja.
