Feitoto aichambua Simba
Kiungo mshambuliaji mahiri wa Azam FC, Feisal Salum Abdallah “Feitoto”, amefunguka kuhusu mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Simba SC, akionya kuwa pambano hilo litakuwa na ushindani mkubwa sana uwanjani.
Feitoto amekiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na kikosi cha Simba kusheheni wachezaji wakubwa na wenye uzoefu mkubwa wa michuano ya ushindani.
Amesisitiza kuwa timu zote mbili zitaingia uwanjani zikiwa na azma moja tu ya kusaka ushindi, jambo ambalo linafanya mchezo huo kuwa wa aina yake.
