Erick Mwijage kuziba pengo la Aziz Ki

Kocha Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, amekuwa akimjenga kiungo mshambuliaji kijana Erick MWIJAGE kwa kumuandaa kisaikolojia kukabili Presha Kubwa za Mechi kubwa ili kuwa muhimili mkubwa wa kikosi cha kwanza cha miamba ya Tanzania, Yanga SC.

Kutokana na ushindani mkubwa uliopo ndani ya kikosi cha Yanga, Mwijage anatazamwa kama dhahabu inayohitaji kusafishwa.

Ingawa anaweza asipate muda mwingi wa kucheza mara kwa mara kutokana na kuwepo na wakali wengine kikosini, kila anapopewa nafasi amekuwa akionesha akili kubwa ya mpira na ukomavu.

Hivi karibuni, msemaji Ally Kamwe, ameweka wazi kuwa Mwijage ndiye anayetarajiwa kuziba pengo la kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki kwenye mchezo mkubwa wa dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba SC.

Hatua hii inathibitisha imani kubwa ambayo benchi la ufundi na uongozi wanayo kwake katika mechi zenye shinikizo kubwa.

MWIJAGE amekuwa mchezaji mwenye uwezo wa kubadilika na kucheza nafasi tofauti za ushambuliaji.

Kocha MANQOBA anamtengenezea Mwijage mazingira ya kujiamini na kuona kuwa ana uwezo wa kubeba timu mgongoni mwake bila hofu.

Manqoba anajulikana kwa kupenda soka la ushirikiano, katika kumjenga Mwijage na wachezaji wengine vijana kama Chuga Boy, kocha huyo amekuwa mkali dhidi ya uchezaji wa ubinafsi, akiwasisitiza kucheza kwa kufuata mfumo wa timu ili kukuza vipaji vyao kwa manufaa ya klabu


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI