Edna Lema ampigia saluti Eng Hersi


Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema, amesema moja ya kumbukumbu kubwa na heshima za kipekee katika safari yake ya soka ni kupata nafasi ya kukaa kwenye benchi la ufundi la Yanga Senior Team akiwa Kocha Mkuu.

Akizungumza kupitia kipindi cha Lavidavi cha Wasafi FM, Edna Lema ameeleza kuwa nafasi hiyo ilikuwa sehemu ya ahadi ya Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said, baada ya Yanga Princess kuifunga Simba SC katika mchezo wa Ngao ya Jamii ya Wanawake.

“Moja ya heshima kubwa kuwahi kupewa kwenye mpira wa miguu ni ile moment ya kuwa Kocha Mkuu. Ilikuwa ni ahadi ya Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said, baada ya timu yetu ya Yanga Princess kuifunga Simba SC kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ya Wanawake.Kwangu ni heshima kubwa sana ambayo amenipa Rais wa Yanga na uongozi wake.”

— Edna Lema, Kocha Mkuu wa Yanga Princess.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI