Dkt Mwinyi apiga ziara ya ghafla mji wa AFCON

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi ametembelea mradi wa Mji wa michezo unaojulikana mji wa AFCON uliopo Fumba mkoa wa Magharibi B Unguja.

Leo nimetembelea na kukagua Mradi wa Mji wa Michezo Zanzibar (AFCON), ikiwa ni sehemu ya ziara zangu za kawaida za kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Katika ziara hiyo, nimekagua miundombinu mbalimbali ikiwemo:

• Uwanja wa mazoezi na uwanja wa mpira wa miguu — sehemu muhimu ya maandalizi ya miundombinu ya michezo.

Mabwawa ya michezo — bwawa la kuogelea lenye urefu wa mita 50 pamoja na bwawa maalum kwa mchezo wa kuruka majini (Diving Pool).

Fan Zone — eneo la wazi lenye uwezo wa kuhudumia watu 4,000.

Miundombinu ya bandari — inayojengwa kwa ajili ya kuhudumia boti ndogo na kubwa.

Awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika tarehe 31 Desemba 2026, hatua itakayoiwezesha Zanzibar kuwa miongoni mwa wenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons