CAF yasisitiza AFCON 2027 ni Tanzania, Kenya na Uganda
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe amesema AFCON 2027 haitaondolewa Tanzania, Kenya na Uganda, akisisitiza kuwa Mataifa hayo yataendelea kuwa wenyeji wa mashindano hayo.
Rais Akizungumza leo Septemba 17, 2026 baada ya kuwasili Tanzania kwa ajili ya kukagua maendeleo ya maandalizi, Motsepe amesema amekuwa akisikia taarifa zinazodai kuwa CAF inaweza kuanza kufikiria mpango mbadala wa kuondoa mashindano hayo katika Nchi hizo tatu.
“Baadhi ya Watu, kutokana na yale ambayo tayari yameripotiwa na baadhi ya Vyombo vya Habari barani Afrika na sehemu nyingine duniani, wanasema Rais wa CAF anapaswa kuanza kufikiria mpango B na mpango C na kuiondoa AFCON Tanzania, Kenya na Uganda, hilo halitatokea,” amesema Motsepe.
“Ninajivunia sana kazi nzuri inayoendelea kufanyika Tanzania, tuna miezi tisa, na moja ya mambo ninayosisitiza ni kwamba tunapaswa kuongeza kasi, tupo hapa kufanya kazi pamoja, kusaidia na kutoa ushirikiano, hii ni AFCON yetu,”
