Bodi ya Wakurugenzi Simba yafanya uteuzi

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC imefanya uteuzi wa wajumbe wa kamati mbalimbali za klabu, kufuatia kikao chake kilichofanyika Septemba 23, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo, Kamati ya Uchaguzi itaongozwa na Anderson David Msumba akiwa Mwenyekiti, huku Alpha Honest Gervas akiwa Makamu Mwenyekiti. Wajumbe wengine ni Rose Manka Sissya, Richard Daudi Mwalwiba na Jotham Mubelwa Mazima.

Kamati ya Nidhamu itaongozwa na Suleiman Hussein Kova akiwa Mwenyekiti, akisaidiwa na Peter Lucas Mwitwa kama Makamu Mwenyekiti. Wajumbe ni Robert Francis Selasela, George Magere Masatu na Racheal Juma Chagonja.

Aidha, Charles Ndalahwa Kenyela ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, huku Anna Anjibithe Marealle akiwa Makamu Mwenyekiti. Wajumbe wengine ni George Rwezaura Shumbusho, Aziz Hassan Kifile na Gerald Robert Yambi.

Uteuzi huo umetolewa rasmi na Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Septemba 24, 2026, ukiweka muundo wa kamati hizo kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu mbalimbali ndani ya klabu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI