Bi Kauye aomba radhi kwa video iliyosambaa
Baada ya Video hiyo pembeni iliyosambaa ya mwigizaji maarufu, Bi Kauye, amejitokeza hadharani kuomba msamaha kwa Watanzania wote kufuatia kusambaa kwa video inayomuonesha akiwa pamoja na kijana mmoja katika mazingira yaliyozua mjadala mkubwa na hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumzia tukio hilo, Bi Kauye amefafanua kuwa kilichotokea hakikuwa na maana kama inavyotafsiriwa na baadhi ya watu, bali kilikuwa ni sehemu ya utani tu wakiwa 'location' wakati wa uandaaji wa kazi ya video.
"Naombeni mnisamehe Watanzania wote. Hayo siyo mambo yangu, ilikuwa ni utani tu tukiwa location. Naombeni mfute hiyo video, mimi nina watoto wakubwa. BASATA pamoja na Bodi ya Filamu naombeni mnisamehe. Hayo siyo mambo yangu kabisa, napitia kipindi kigumu mno," alisema Bi Kauye kwa majuto.
Bi Kauye amewataka Watanzania kutomuhukumu kwa kile kinachoonekana kwenye video hiyo, huku akisisitiza kuwa mazingira yaliyokuwa yanaendelea yalihusisha utani wa kikazi wakati wa utengenezaji wa video na sio maisha yake halisi.
