Aziz Ki aiponza Yanga

Baada ya mchezo wa Ligi Kuu NBC PL 2026/27 kumalizika dhidi ya Geita FC, ambapo klabu ya Yanga ilipata ushindi wa bao moja bila, huku mchezaji wa klabu hiyo, Aziz Ki, akipokea adhabu ya kadi nyekundu baada ya kufanya madhambi.

Sasa, kupitia mchezo huo, mashabiki wa klabu ya Yanga walianza kufanya fujo nyingi kufuatia tukio la ushangiliaji. Mashabiki wa klabu ya Yanga walikutwa wakifanya kosa la kuwapiga mashabiki wa klabu pinzani ya Geita FC kwa chupa za maji.

Kufuatia tukio hilo, kwa mujibu wa taarifa ya leo, Septemba 19, 2026, uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) umeitoza klabu ya Young Africans faini ya Tsh milioni tano kwa kosa la kuwapiga kwa chupa za maji mashabiki wa timu pinzani.

Tukio hilo, licha ya klabu hiyo kupigwa faini, limepewa onyo kubwa mno ndani ya taarifa hiyo, kama ilivyotolewa na Mratibu wa Mchezo kwenye mchezo huo, kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:15 kuhusu Taratibu za Mchezo. Wakati wa kupasha misuli joto (Warm Up), wachezaji watatu wa klabu hiyo waliingia uwanjani saa 12:00 jioni badala ya saa 12:10 jioni.

Michezo hiyo imekuwa ikifuatiwa na kitendo hicho kujirudia mara kadhaa, huku TPLB ikiweka mkazo kuwa endapo kitajitokeza tena, hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Katika hatua nyingine, Afisa Ulinzi na Usalama wa Yanga, Eddie Evance, amepelekwa kwenye Kamati ya Maadili ya TFF kwa madai ya kukaidi kutekeleza maamuzi ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, baada ya kuonekana uwanjani licha ya kuwa anatumikia adhabu ya kutokuingia uwanjani kwa vipindi sita, iliyotolewa Juni 8, 2026.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI