Al Ahli Tripoli yaisurubu bila huruma KMKM
Fiston Kalala Mayele na wenzake wameonyesha ubora mkubwa baada ya kuichapa KMKM 3-0 kwenye Uwanja wa New Aman Complex.
Al Ahli Tripoli wameanza kwa kishindo safari yao ya CAF Confederation Cup, huku Mayele akiendelea kuonyesha makali yake!
Mabao mengine ya Tripoli yamefungwa na Mahdou El Houni dakika ya 20 na Hocine Dehiri dakika ya 27, Mayele akifunga dakika ya 22
KMKM sasa wana kazi kubwa ya kwenda kupindua meza ugenini kwenye mchezo wa marudiano
