Ajali ya bodaboda yaondoa uhai kipa wa Azam FC U20


MCHEZAJI wa Azam FC U-20, Iddy Salim, amefariki dunia baada ya kupata ajali ya pikipiki jana Alhamisi, Septemba 10, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Klabu ya Azam FC, marehemu alikuwa akicheza nafasi ya kipa katika timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (U-20).

Mwili wa marehemu kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala (MRRH), ambapo unafanyiwa taratibu za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Tanga kwa ajili ya maziko.

Azam FC pia imetuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kufuatia msiba huo.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI