UKRISTO NI CHIMBUKO LA UYAHUDI - 9

Inaandikwa na Fikiri Salum

Ilipoishia 

WA kwanza kuuawa alikuwa Stefano, na kati ya mitume Yakobo mkubwa kabla ya kufa wengi kwa kuuawa, mitume waliweza waandamizi wao, ambao kati yao Maaskofu mwanzoni mwa karne ya 2 walikuwa wameshika uongozi wa Makanisa wakisaidiwa na Mapadri na Mashemasi.

Endelea

Wakati huo huo vitabu vingi vya Wakristo vilivyotungwa katika nusu ya pili ya karne ya 1 vilizidi kuenea na kukusanywa hadi vikaunda Agano jipya.

Baada ya hapo vitabu viliendelea kuandikwa kwa kutetea, kutangaza na kufafanua imani sahihi, ndiyo mwanzo wa teolojia za ufafanuzi huo, kama zile kati ya shule ya Aleksandra na shule ya Antiokia, ndizo chanzo cha mabishano yaliyochangia mabishano makubwa yalitokea hasa katika karne ya 5.

Ingawa kuanzia mwaka 325 mitaguso mkuu ilikusanya Maaskofu wengi kutoka sehemu mbalimbali kumaliza mgogoro- tofauti za lugha na utamaduni, pamoja na utaifa, zilichangia sana mafarakano.

Maendeleo mengine muhimu yalipatikana katika maisha ya kiroho kwa uanzishaji wa Umonaki wa Kikristo, kwanza katika majangwa ya Misri, halafu sehemu nyingine zote.

Juhudi za watu hao zilichochea waumini wenzao pia kuwa waaminifu katika ulimwengu uliozidi kuwashawishi badala ya kuwatesa.

Ni kwamba kufikia mwisho wa karne ya 4 Ukristo ulikuwa dini rasmi ya dola la Roma ambalo kabla ya hapo kwa miaka karibu 250 (64- 313) lilikuwa limeukatwza kikatili.

Kabla yake Armenia ilikuwa nchi ya kwanza kupokea Ukristo kama dini ya taifa (301) ushindi huo ulifanya wengi watamani vyeo ndani ya kanisa, kwa kuwa viliendana sasa na heshima na malii hivyo ubora ulipungua.

Dola la Roma magharibi ulipozidi kudhoofiwa na uvamizi wa Wagermanik na makabila mengine yasiyostaarabika, Askofu' wa Roma kama mchungaji mkuu alilazimika kuwajibika Ili kuokoa jahazi.

Ndivyo walivyofanya hasa Papa Leo 1 na Papa Gregori 1, kwa juhudi za Wamonaki, Wabenedikto na wengineo, ustaarabu wa kale uliokosewa katika vitabu vyake na uinjilishaji uliendelea katika Ulaya ya kati.

Kumbe, uenezi wa Uislamu kuanzia karne ya 7 ulidhoofisha na pengine kukomesha kabisa Ukristo katika nchi nyingi, ukirudisha nyuma ustawi wa kanisa lote.

Hata hivyo mwanzoni mwa karne ya 8 Uislamu ulizuiwa na Wafaranki, kuenea zaidi bara Ulaya, kabila hilo kubwa la Kijerumanik liliwahi kujiunga na kanisa katoliki likawa msaada mkubwa kwa Mapapa.

Isipokuwa kwa kuwaachia watawale Italia ya kati walisababisha Papa aanze kuwa kama Mfalme wa dunia hii, jambo lililoathiri sana majukumu yake ya kiroho hadi mwaka 1870.

INAENDELEA 




Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons